Naamini mtu akitoa hit ana kitu – Ditto
Msanii wa Bongo Flava, Ditto amesema mitandao ya kijamii ina nguvu kubwa katika kumsaidia msanii kufanya vizuri lakini haiwezi kuwa sababu ya kutengeneza hit song.
Hitmaker huyo wa ngoma ‘Moyo Sukuma Damu’, ameeleza hits song haiwezi kupatikana kutokana na mitandao ya kijamii bali ni ubunifu na uwezo binafsi wa msanii.
“Mimi naamini mtu aki-hit ana kitu, uwe mkubwa, uwe Ditto, uwe mdogo, uwe sijui nani wimbo wako lazima uwe na kitu, ukikataa hauna kitu, lakini hata ukikataa sio mwisho wa dunia ilimradi una kipaji na uwezo endelea kupigana, kurekodi na toa nyimbo nyingine,” ameiambia E-Newz ya EATV.
Alipoulizwa kama kiki zinaweza kupelekea msanii kutengeneza hit song alisema, “ilimradi unawafikia watu wako, kazi yako inakwenda na malengo yako unayafikia, sidhani kama ni jambo baya. Binafsi naamini kwenye kazi ninapokuwa narekodi, ninapoandika nataka kazi iwe nzuri,” amesisitiza.
No comments