Rooney;Everton wamefurahia ukarimu wa Watanzania
Timu ya Soka ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uiungereza imemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania na kueleza kufurahishwa na namna Watanzania walivyoipokea timu hiyo.
Wayne Rooney (wa tatu kushoto) akiwa na wachezaji wenzake walipokuwa Jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Everton ilicheza na timu ya Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki ulichezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Timu ya Everton iliwasili Tanzania siku ya Jumatano wiki hii ambapo juzi ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.
“Nimepata uzoefu mpya kwangu kuja hapa (Tanzania) na nina tumaini sasa Makamu wa Rais atakuwa akiishabikia Everton”, alieleza Wayne Rooney kupitia tovuti ya timu hiyo.
Pia katika akaunti yake ya mtandao wa tweeter, Rooney aliwashukuru mashabikji wa Tanzania kwa kuiunga mkono Everton katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.
“Great start to the pre-season. Special thanks to the fans supporting us in Tanzania”, aliandika Rooney akitoa shukrani za pekee kwa Mashabiki wa Tanzania.
Kwa upande wa Kocha wa timu hiyo, Ronald Koeman alielezea kufarahia ziara ya kuja Tanzania na zaidi ni kutokana na hali ya urafiki iliyooneshwa na mashabiki wa soka nchini.
Rooney pia aliungana na wachezaji wengine kama Morgan Schneiderlin, Jonjoe Kenny na Kevin Mirallas wa timu hiyo walipata fursa ya kujifunza tamaduni za kimsai, kujifunza kupika chakula cha asili, kutembelea shule yenye wanafunzi wenye mahitaji maalum na pia kufanya mazoezi na timu ya vijana wenye ulemavu wa ngozi (Albino United).
Timu ya soka ya Everton ilifanya ziara nchni Tanzania ambapo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, Marais wastaafu, Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
No comments