Nina ofa ya ngoma 10 kutoka kwa Trey Songz – Ben Pol
Msanii wa RnB Bongo, Ben Pol ameweka wazi mipango yake ya kufanya ngoma na wasanii wa nje.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Bongo Flava Top 20 cha EA Radio kuwa kutokana na ngoma yake ‘Tatu’ aliyomshrikisha Darassa kufanya vizuri amejikuta akipata ofa mbalimbali za kufanya kazi na wasanii wakubwa wakimataifa kama Chidinma wa Nigeria na Trey Songz wa Marekani.
“Nina kolabo nyingi zinakuja, nimeshafanya moja na Chidinma wa Nigeria ipo tayari, pia nina ofa ya ngoma 10 kutoka kwa director wa msanii Trey Songz wa Marekani ambapo nitaweza kufanya kazi moja na Trey Songz,” amesema Ben Pol.
No comments