Rais wa Shirikisho la soka Hispania ajiuzulu nyadhifa zake zote baada ya tuhuma za rushwa
Rais wa Shirikisho la Soka nchini Hispania (FA), Angel Maria Villar amejiuzuru nafasi yake ya makamu wa rais wa Uefa na Fifa.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini Hispania (FA), Angel Maria Villar
Villar na mtoto wake wa kiume, Gorka walikamatwa na Takukuru ya Hispania inayojulikana kama Unidad Central Operativa mwanzoni mwa mwezi huu kwa tuhuma kadhaa zikiwemo za matumizi mabaya ya ofisi, tuhuma za rushwa na nyingine zinazoelezwa kusababisha wizi wa fedha.
Villar, ambaye alikanusha tuhuma hizo dhidi yake amesimamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Hispania kwa mwaka mmoja.
Chama cha Mpira wa Miguu barani Ulaya (Uefa ) kwenye taarifa zake leo Alhamisi kimesema,Villar hatakuwa na kazi yeyote tena katika shirika hilo.
“Villar hatakuwa na kazi yeyote katika shirika hili, kwa kuzingatia kesi ambazo zinaendelea kumkabili nchini Hispania hatuna lakufanya tena ju ya hili” imesema ripoti kutoka Uefa leo.
Rais wa Uefa, Aleksander Ceferin amekubali kujiuzuru kwa Villar na kumshukuru kwa muda wake wote aliyotumia kutumikia soka la Ulaya.
Villar, ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Athletic Bilbao na kiungo wa timu ya taifa ya Hispania ameliongoza Shirikisho la Mpira wa Miguu la Hispania kwa miaka 29 .
No comments