Rihanna atarajia kuja Afrika mwaka huu
Msanii wa muziki wa Pop na RNB nchini Marekani, Rihanna amekutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na mkewe Brigitte Macron, jijini Paris kwa ajili ya kutoa misaada kwa Bara la Afrika katika elimu.
Mwezi wa pili mwaka huu, msanii huyo alitunukiwa tuzo ya ‘Humanitarian of the Year’ na chuo cha Harvard kwa mchango wake katika elimu na afya.
Akizungumza na waandishi masanii huyo amelezea mipango yake ya kusaidia katika elimu kupitia tasisi yake. “Nilikuwa na kikao kizuri na Rais wa Ufaransa na mkewe.Wamenikaribisha na tumeongea kuhusu mada ya elimu tutatangaza tuliyoyafikia ifikapo Septemba mwaka huu,” amesema Rihanna.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwanamuziki Rihanna
Pia mrembo huyo ametangaza kurejea Afrika ifikapo Oktaba mwaka huu, kwa ajili ya kuendelea na mipango yake ya kusaidi Bara hilo katika elimu.
Rihanna na mke wa Rais wa Ufaransa Bi.Brigitte Macron
Mwezi wa pili mwaka huu, msanii huyo alitunukiwa tuzo ya ‘Humanitarian of the Year’ na chuo cha Harvard kwa mchango wake katika elimu na afya.
No comments