Tanzania na Kenya zakubaliana kuondoa vikwazo vya kibiashara
Serikali za Tanzania na Kenya zimekubaliana kuondoa vikwazo vya kibiashara zilizokuwa zimewekeana kuhusu bidhaa kutoingizwa baina ya nchi hizo mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga ameeleza kuwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo ni kuzingatia taratibu za kibiashara ambazo zilikubaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Dkt Mahiga,amesema Tanzania na Kenya zimemaliza tofauti za kibiashara zilizojitokeza karibuni ” Juhudi za awali za serikali ya Tanzania ilikuwa ni kuona vikwazo hivyo vinaondolewa na Kenya kwa wakati lakini hazikuzaa matunda. Hali hiyo ilisababisha Tanzania nayo kuweka vikwazo kwa bidhaa za maziwa na sigara kutoka Kenya zisiingie katika soko la Tanzania,” alisema Mahiga.
“Kwa kuzingatia mahusiano mazuri ya kindugu yaliyopo kati ya nchi hizi mbili na kwa kujali manufaa mapana ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, viongozi wakuu wa nchi hizi mbili Dkt. John Magufuli na Uhuru Kenyatta wa Kenya walikubaliana kuviondoa vikwazo hivyo mara moja.”
No comments