Video: Navy Kenzo kuanza tour Europe, Australia na Marekani
Kundi la Navy Kenzo linalofanya vizuri katika Bongo Flava, wamebainisha kuendelea na tour yao Europe, Australia na Marekani.
Navy Kenzo ambao kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma yao mpya ‘Bajaj’ ambayo wamemshirikisha Patoranking, wamesema kufanya tour nje ya nchi ni ishara kuwa muziki wao umekua.
“Tutaendelea Europe, tutaenda Australia na vile vile tutaenda Marekani, Europe yetu ilikuwa ianze July mpaka October lakini tumesogeza mbele kidogo kwa hiyo tutatangaza new date na watu wataona,” amesema Nahreel.
Pia Aika ameongeza kuwa, “Sisi kama wasanii nyimbo zetu kuvuka mipaka ni mafanikio makubwa sana ina maanisha fan base yetu ni kubwa, albamu yetu imeweza kufika nchi nyingi sana ni kitu ambacho kinatushangaza na kwetu Tanzania unakuta hata watu hawajawahi kuitangaza”.
April mwaka huu kundi hilo lifanya tour nchini Israel na Nahreel amesema tour hiyo ilikua yenye mafanikio makubwa, “ni nchi ambayo hawaongei kingereza wala hawajui Kiswahili, tulivyoenda tumekuta Kamati inaimbwa na tulifanya matamasha manne, kwa kweli watu walikuja na sisi tulishangaa,” amesisitiza.
No comments