Mwandishi Adebayo afariki dunia
Mwandishi mkongwe wa mashairi aliyeitafsiri nyimbo ya taifa ya Nigeria kutoka kwa lugha ya Kiingereza kwenda kwa lugha ya Yoruba, Adebayo Faleti amefariki dunia.
Adebayo ambaye alikuwa na miaka 86, amefariki siku ya jana akiwa katika hospitali ya University College Hospital Ibadan, Marehemu pia alikuwa akifanya kazi ya uigizaji na uandishi wa habari nchini humo.
Enzi za uhai wake marehemu amewahi kupata tuzo mbalimbali za kimataifa ikihusisha tuzo ya heshima kutoka ofisi za serikali katika nchi hiyo, vile vile mwaka 1995 katika tamasha la sanaa alipata tuzo ya Eda Ko L’aropin na kwenye Afro-Hollywood Award alipata tuzo ya Outstanding Performance katika Arts.
No comments