Nina ndoto za kuwa zaidi ya WCB – Aslay
Msanii wa Bongo Flava, Aslay amesema hana mpango kuwa chini ya record label yoyote Bongo kwa sasa kutokana mipango yake ni mikubwa zaidi.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Baby’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa mipango yake ni kufikia kiwango cha Diamond na Alikiba.
“Kusainiwa WCB hapana, kwa sababu mimi nina ndoto za kuwa zaidi ya WCB au kuwa zaidi ya kitu kingine chochote, naamini nitakaza nitafika hizo sehemu, naweza kusema nina ndoto za kufika kama alipofika Chibu, nina ndoto za kufika kama alipofika Alikiba,” amesema na kuongeza.
“Inabidi nikaze niwe mimi kama mimi nitafute njia ya kutoboa nifike level hiyo, yaani sio yeye pekee yake mtu yeyote, wakisema wanisaini siwezi kukubali sasa hivi,” amesisitiza Aslay.
No comments