USAJILI: Chelsea yahitaji kuwasajili wachezaji hawa kwaajili ya msimu ujao
Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza inahitaji kumsaini mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang baada ya kumkosa mchezaji Romelu Lukaku.
Klabu ya Chelsea inamuhitaji mshambuliaji, Pierre-Emerick Aubameyang katika kipindi hiki cha majira ya joto
The Blues inahitaji kusajili mshambuliaji mwenye kiwango cha hali ya juu katika kipindi hiki cha majira ya joto mara baada ya mchezaji wao Diego Costa kutarajiwa kuondoka Stamford Bridge.
Antonio Conte amemuambia mchezaji, Diego Costa atafute pakwenda katika kipindi hiki cha usajili
Meneja wa Chelsea, Antonio Conte anatamani kuwapata wachezaji, Aubameyang Alvaro Morata wa Real Madrid na Torino Andrea Belotti.
Chelsea pia inahitaji saini ya mshambuliaji wa Madrid, Alvaro Morata
Dortmund itamuachia mchezaji wake Aubameyang katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya joto kwa dau la pauni milioni 70 na tayari mchezaji huyo ameshaiambia klabu hiyo kuwa anahitaji kuondoka.
Matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain na AC Milan zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28.
Mtendaji Mkuu wa Dortmund, Hans-Joachim Watzke amesema mpaka sasa hakuna ofa yoyote iliyofika mezani na hivyo amewahasa wanaomtaka mchezaji huyo kwenda na muda.
No comments