Vita ya kiuchumi ni mbaya – Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa vita ya kiuchumi ni mbaya ambapo amesema vita hiyo wakubwa huwa hawafurahi ila Watanzania wema watasimama kuliombea taifa hili.
Rais Magufuli ameyasema hayo jana wakati akizungumza katika ziara yake wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Kibondo-Nyakanazi.
“Naniliwaambia nimeanzisha vita ya kiuchumi, vita ya kiuchumi ni mbaya sana, ni mbaya sana wakubwa wale huwa hawafurahi kuna viongozi wengine tu mmeona yaliyo wapata ni kwasababu nchi zao zilikuwa na mali, lakini wale wakubwa wakataka kuchezea hizo mali kwa yao na si kwa wananchi wa pale, walitumia mbinu nyingi za kila namna lakini nataka niwaambie ndugu zangu Mungu wangu ni mwema nawa Tanzania wema watasimama kwaajili ya kuliombea taifa hili,” alisema Rais Magufuli.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli alisema wawekezaji walioitwa kuzungumza na serikali wakichelewa ataifunga migodi yote.
No comments