Usikose Hizi Hapa

Rais Magufuli Ampongeza Kagame kwa Kuchaguliwa Tena Kuwa Rais

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametangazwa mshindi wa Urais wa nchi hiyo baada ya kushinda katika uchaguzi Mkuu uliofanyika  August 4, 2017 na kumrudisha madarakani kwa muhula wa tatu.
Baada ya ushindi huo Rais wa Tanzania John Magufuli ametumia ukurasa wake twitter kumtumia salamu za pongeni Rais Kagame.

”Nakupongeza Mhe. Paul Kagame kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Rwanda kwa kipindi kingine. Kwa niaba ya Watanzania wote nakutakia mafanikio mema.

"Tutaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano na uhusiano kati ya nchi zetu hususani biashara na maisha ya wananchi wetu. Hongera Wanyarwanda. "


No comments