Usikose Hizi Hapa

Azam FC wapo tayari kumvaa ‘mnyama’ Simba SC

Kuelekea mchezo wa Azam FC v Simba SC, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema kuwa kikosi chao kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo na wanaamini watapata ushindi kwa jinsi walivyojipanga kwenye idara zote.
Timu hizo zinakutana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex ikiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo timu hizo zitaumana kwa mara ya kwanza uwanjani hapo baada ya Azam kuruhusiwa kuutumia uwanja huo katika mechi dhidi ya Simba na Yanga.
Tunawaheshimu wapinzani wetu, Simba ni timu nzuri na tunatarajia mchezo utakuwa mgumu, lakini tunaamini pia ubora wa kikosi chetu na maandalizi ni silaha yetu nzuri ya ushindi siku hiyo.”amesema Maganga.
Kwa upande mwingine, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amesema kuwa mchezo huo wanauchukulia umuhimu licha ya kuwa ni kama michezo mingine wanayocheza kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Huu ni mchezo wetu wa pili wa ligi na tunahakikisha tunacheza nyumbani na uwanja wetu wa nyumbani tunataka tushinde kwa sababu toka tumefungua uwanja wetu huu tumewahi kupoteza mara tatu tu na hatutegemei kupoteza tena katika msimu huu, Kwa hiyo kwanza ni kitu cha umuhimu kwamba tuweze kushinda nyumbani, halafu mwaka huu tuna dhamira ya kufanya mambo makubwa zaidi,” amesema Nassor Cheche huku akielezea maandalizi ya safu ya ushambuliaji ambayo mchezo uliopita dhidi ya Ndanda FC ilionekana kupoteza nafasi nyingi.
Mchezo wa mpira ulivyo ni mchezo wa makosa, hauwezi kuwa bora kila siku, tumeanza vizuri katika safu ya ulinzi na kiungo, matatizo katika ushambuliaji na sasa hivi tumelifanyia kazi sana hilo na kuhakikisha na yale tuliyofanya nyuma katika kiungo na ulinzi yasije yakabadilika, kwa hiyo tumehakikisha idara zote zinakaa vizuri ili kutupa matokeo mazuri katika michezo yetu kuanzia huu na mingine inayokuja mbele,” .

No comments