Usikose Hizi Hapa

Wanarudi Chamazi kama Wageni

Katika safari ya maisha ya mpira huwa kuna vipindi vya usajili, vipindi hivi ndivyo wachezaji huwa wanaamua jinsi ambavyo maisha yao yatakavyokuwa kutokana na kuwa ni kipindi ambacho wanapiga pesa.
Kesho klabu ya Azam inakutana na klabu ya Simba katika uwanja wa Chamazi, lakini kuna wachezaji wa Simba ambao ni wenyeji katika uwanja huo na wanarudi wakiwa kama wageni.
Simba iliwasajili Erasto Nyoni, Aishi Manula, Shomari Kapombe na John Bocco kutoka katika kikosi cha kwanza cha Azam FC, huku wengi wao walikuwa tayari ni wenyeji ndani ya uwanja huo, mazingira yote yanayohusu kwa namna moja ama nyingine klabu ya Azam.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa pande zote mbili, kutokana na wachezaji walioondoka Azam, watataka kuonyesha kuwa wameondoka na bado wapo katika kiwango cha juu.
Vile vile klabu ya Azam watataka kuonesha usajili wao ambao wameufanya ni usajili sahihi na hata hao walioondoka hawajaacha pengo lolote katika kikosi chao.
Azam wana kikosi kilichojaa nyota vijana, ambao wanataka kuonekana na kufanya mambo makubwa, hivyo wanaweza wakafanya lolote katika mechi hiyo.
Nyoni, Manula na Bocco wanaweza wakawa katika kikosi kitakachoanza, katika mechi hiyo huku Shomari Kapombe akiwa jukwaani kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Wachezaji hawa wanarudi wakiwa kama wageni, kwa kucheza ugenini lakini mazingira ya Chamazi na miundombinu ni ile ile ambayo waliiacha.

No comments