Wanafunzi darasa la 3 wafariki wakichimba mchanga
Wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Chikomo Tarafa ya Nalasi, Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma, Selina Selemani Kazembe (12) na Sofia Sillo (9) wote wa darasa la tatu wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa shimo la mchanga waliokuwa wakichimba kwa ujenzi wa darasa.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa mkoani Ruvuma SACP Geminy Mushi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Wanafunzi wa hawa walipoteza maisha na ukuta wa shimo la mchanga walipokuwa wakichimba mchanga kwaajili ya ujenzi wa darasa la shule, kazi hiyo walikuwa wanafanya kama sehemu ya mafunzo yao yaitwayo kama elimu ya kujitegemea kilichotokea baada ya wanafunzi hao kuangukia wa mchanga na kupoteza maisha palepale, mchanga uliwafukia na kuangukia sehemu ya kifuani jitihada za kuwatoa na walifikishwa katika hospitali ijulikanayo kama Mbesa bahati mbaya wakawa wamepoteza maisha,” alisema SACP Mushi.
Kamanda huyo amesema jitihada zilizofanyika ni kuwakimbiza watoto hao katika hospitali ya Mbesa lakini kwa bahati mbaya walikuwa wamepoteza maisha.
No comments