Mbunge Esther Bulaya Atiwa Mbaroni
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Esther Bulaya amekamatwa na jeshi la Polisi akiwa katika Hotel ya Kifa Best Point Wilayani Tarime akidaiwa kujiandaa kutaka kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.
Kamanda wa polisi Tarime/Rorya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Henry Mwaibambe amesema wabunge Bulaya na John Heche hawatakiwi kujumuika kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo ka Tarime.
No comments