Watu 60 wafariki dunia katika maporomoko ya ardhi DR Congo
Watu takribani 60 wamefariki dunia katika maporomoko ya ardhi yaliyotokea karibu na Ziwa Albert huko Kaskazini Mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo Jumatano hii.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Al Jazeera, limeripoti kuwa watu wengi waliofariki katika tukio hilo ni kutoka katika kijiji cha Ituri ambacho kipo karibu na Ziwa hilo.
Inadaiwa kuwa sababu ya vifo hivyo vimetokana na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha na kusababisha mlima uliopo karibu na eneo hilo kukatika na kufunika katika eneo la kijiji hicho.
Aidha inaelezwa kuwa watu wengine wamefariki wakati wakitafuta dhahabu kwenye migodi ya zamani.
No comments