Usikose Hizi Hapa

Watu wenye matatizo ya uhafifu wa kuona na upofu kuongezeka duniani

Idadi ya watu wanaopata matatizo ya kuona kwa uhafifu au upofu duniani inakadiliwa kuongezeka duniani huku sababu zikitajwa kuwa ni mabadiliko ya hali ya hewa na mtindo wa maisha.
Tokeo la picha la blind people
Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa na jarida la afya la Lancet linatabiri kuwa watu watakaopata upofu au matatizo ya kuona kwa uhafifu  wataongezeka kutoka milioni 36 waliopo sasa na kufikia watu milioni 115 ifikapo mwaka 2050 kama matibabu hayataboreshwa.
Watafiti hao wanasema idadi ya watu duniani wanaokabiliwa na tatizo la kutokuona vizuri limepungua katika miaka ya hivi karibuni lakini idadi hiyo inaweza kubadilika kutokana na mitindo tofauti tofauti ya maisha ikiwemo urembo wa macho, aina ya vyakula, ongezeko la joto na idadi ya watu duniani.
Maeneo yanayotajwa kukumbwa  na matatizo hayo ni Kusini na Mashariki mwa bara la Asia huku nchi za eneo la kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika nazozikitabiriwa kuathiriwa na janga hilo.

No comments