Usikose Hizi Hapa

Picha: Zamaradi Mketema afunga ndoa kimya kimya

Mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema amefunga ndoa wiki hii na kijana anayedaiwa kuwa ni mtoto wa kigogo.
Mrembo huyo ambaye ni mama wa watoto wawili, amepost picha akiwa mtandaoni akiwa na mwanaume huyo aliyefunga naye na kuandika ujumbe wa kumshukuru mungu.
“ALHAMDULILLAH!!,” aliandika Zamaradi baada ya kupost picha hiyo hapo juu.
Rafiki wa karibu wa Zamaradi, Faiza Ally amempongeza rafiki yake huyo kwa kumtakia maisha marefu katika ndoa yake.
“Bismalah mashallah @zamaradimketema ndoa yako iwe ya kheri Inshallah,” aliandika Faiza Ally.
Wadau wa mambo wanadai mume wake huyo ni mtoto wa Kigogo mzito na inadaiwa wamekuwa pamoja kwenye mahusiano kwa miaka kadhaa sio wa kukurupukia ndoa kama wengine wanavyodhani.

No comments