Barcelona kuhamia Ligi kuu nchini Uingereza ?
Wanachama wa klabu ya Barcelona watalazimika kuamua ni ligi ipi watahitaji kwenda kucheza endapo kama Catalonia itapata uhuru wake kutoka Hispania hayo yamesemwa na rais wa timu hiyo, Josep Maria Bartomeu hapo jana siku ya Jumatatu.
Klabu hiyo inayotoka katika Jimbo la Catalonia siku ya Jumapili imecheza mchezo wake wa Ligi Kuu nchini Hispania ‘La Liga’ dhidi ya Las Palmas bila ya mashabiki kufuatia vurugu za baadhi ya wakazi kuhitaji kupiga kura ya kujitenga na nchi hiyo wakati Serikali ikizuwia zoezi hilo kwa kutumia askari, Barca ilichomoza na ushindi wa mabao 3-0.
“Kwa swala la uhuru wa Catalonia klabu na wanachama wake watapaswa kuamua tutapenda kushiriki kucheza,” amesema rais wa klabu ya Barcelona Bartomeu baada ya kikao cha wanachama.
Rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu
Josep Maria Bartomeu “Tunapitia kipindi kigumu na tutalazimika kuheshimu kile kitakachotokea na kuwa watulivu.”
Waziri wa michezo wa Catalonia,Gerard Figueras wiki iliyopita amesema klabu ya Barcelona inaweza kushiriki Ligi za nchi nyingine kama endapo watapata uhuru kutoka Hispania.
“Kuhusiana na swala la Uhuru timu zote za Catalonia zinazoshiriki La Liga Barcelona, Espanyol na Girona wataamua wapi watapenda kwenda kucheza kama ni hapa Hispania, ama nchi za jirani kama Itali, Ufaransa hata Ligi Kuu ya nchini Uingereza,” amesema waziri wa michezo, Figueras.
No comments