Usikose Hizi Hapa

HATIMAYE MAREKANI NA ISRAELI ZAJIONDOA KATIKA UNESCO

Marekani na Israel zimetangaza kujiondoa kutoka shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO zikidai Israel inabaguliwa.
Marekani na Israel zimetangaza kujiondoa kutoka shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO zikidai Israel inabaguliwa
Wizara ya mambo ya kigeni ilisema kuwa itabuni ujumbe wa waangalizi kwenye shirika hilo lenye makao yake nchini Ufaransa kuchukua mahala pa uwakilishi wake.
Mkuu wa Unesco Irina Bokova, amesema amesikitishwa lakini hajashangazwa.
Tangu wakati wa kampeni zake Trump alikuwa akitoa matamshi ya kuubeza Umoja wa mataifa na pia kulalamika kwamba Marekani ndio inayochangia fedha nyingi zaidi, hivyo kukariri kwamba atapunguza mchango wake.
Mwaka 2011 Marekani ilifuta bajeti yake kwa Unesco kupinga hatua yake ya kuwapa Wapalestina uanachama kamili.
Marekani hutoa asilimia 22 ya bajeti ya kawaida ya Umoja wa Mataifa na asilimia 28 kwa shughuli za amani za Umoja wa Mataifa.
Unesco iko katika mikakati ya kumteua kiongozi mpya huku mawaziri wa zamani wa Qatari na Ufaransa, Hamad bin Abdulaziz al-Kawari na Audrey Azoulay wakiwa mstari wa mbele katika ushindani huo wa ni nani atachukua mahala pake bi Bokova.

No comments