Usikose Hizi Hapa

KENYATTA AKUTANA NA MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI, IEBC

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amekutana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, IEBC, kabla ya uchaguzi mpya uliopangwa kufanyika siku ya Alhamisi Oktoba 26.

Wiki iliyopita Mwenyekiti huyo Wafula Chebukati alikutana na kiongozi wa Muungano wa Upinzani, Nasa, Raila Odinga.

Mapema wiki iliyopita Bw. Chebukati aliomba mazungumzo ya moja kwa moja kati ya rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga. Mazungumzo ambayo yalipuuziwa na rais Kenyatta.

Raila Odinga alitangaza kutoshiriki uchaguzi wa Oktoba 26. Lakini baada ya kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, alilegeza msimamo na kusema anaweza kubadilisha mawazo na kurejea kwenye kinyang'anyiro hicho iwapo kutakuwa na mazungumzo na kufanyika kwa mageuzi ndani ya Tume ye Uchaguzi.

Bw. Chebukati ameviambia vyombo vya habari kwamba anapanga kuwakutanisha Raila Odinga na Uhuru Kenyatta kabla ya uchaguzi mpya wa urais Alhamisi wiki hii.

No comments