Rais Trump abanwa na Wamarekani kuhusu shambulizi la Las Vegas
Rais wa Marekani Donaldo Trump amekosolewa vikali kwa kitendo cha kutuma salamu za rambirambi kwa watu 50 waliofariki kwenye tukio la shambulio la kigaidi jana usiku mjini Las Vegas, Marekani.
Trump ameandamwa na wamarekani wakimtaka atamke tukio hilo kama shambulizi la kigaidi na sio tukio linalohusiana na ishu za ubaguzi wa rangi huku wakimhimiza afanyie marekebisho sheria za umiliki wa silaha za moto.
Baadhi ya watu wamemkosoa vikali Rais Trump kwa kumwambia afute msimamo wake wa kuwazuia waislamu kuingia Marekani akiamini kuwa waislamu ndio wanaotekeleza mashambulizi ya kigaidi wakati mtu yeyote anaweza kuwa gaidi.
Hata hivyo, watu wengi wameonekana kukerwa zaidi na salamu za rambi rambi alizozitoa Rais Trump mapema leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Haya ni baadhi ya maoni ya Wamarekani walioonesha kukerwa kwa Rais Trump kwa kushindwa kutangaza kuwa shambulio hilo ni la kigaidi.
Mpaka sasa hivi watu 58 wameripotiwa kufariki dunia kwenye tukio hilo na kundi la ISIS limekiri kwa namna moja kuhusika na shambulizi hilo huku serikali ya Marekani ikisuasua kuweka wazi taarifa hizo.
No comments