WENGER AINGIA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA KOCHA BORA WA MWEZI
Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameingia katika orodha ya makocha bora wanao wania tuzo ya mwezi Septemba Ligi Kuu nchini Uingereza na kuungana na Jose Mourinho.
Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger
Wenger ameiyongoza the Gunners kushinda jumla ya michezo miwili na kusuluhu mmoja mwezi uliyopita hivyo kuingia katika orodha ya makocha wanne wanao wania tuzo hiyo ya mwezi uliyopita.
Manchester City, ambayo inaongoza Ligi Kuu nchini Uingereza ndiyo timu pekee iliyofunga michezo yake yote minne mwezi uliyopita na kumfanya kocha, Pep Guardiola kuwa miongoni mwa wanao wania tuzo hizo.
Jose Mourinho ameiyongoza Manchester United kushinda jumla ya michezo mitatu na kutoka suluhu mmoja na hivyo kushika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kwa kutofautiana goli moja dhidi ya vinara Man City hivyo anakuwa kocha mwingine anayewania tuzo hizo.
Mauricio Pochettino anahitimisha idadi ya makocha wanao wania tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwezi na EPL mpaka sasa amejikusanyia jumla ya pointi 10 kati ya 12 mwezi Septemba.
Msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza
No comments