WADAU ZAIDI YA 500 KUJADILI CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA AFYA
Zaidi ya wadau 500 wa Afya kutoka ndani na nje ya
Tanzania, wanatarajia kukutana na kujadili changamoto zinazoikabili Sekta ya
Afya na kupata mapendekezo yatakayosaidia Serikali katika kuboresha huduma za
Afya nchini.
Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Tanzania
Health Summit unatarajia kufanyika kuanzia Novemba 14 hadi 15 mwaka huu,Katika
ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere ,jijini Dar es Salaam.
Rais wa Taasisi hiyo Dokta Omary Chillo amesema
pamoja na mambo mengine,mkutano pia utajadili vifo vya mama na watoto,namna ya
kupunguza ugonjwa malaria ifikapo mwaka 2020,ubunifu wa vitendea kazi na
viwanda katika sekta ya Afya.
Mkutano huo utahusisha wataalamu wa
afya,watunga sera,watafiti wa magonjwa ya Afya,wachumi,wasambazaji wa vifaa
tiba na dawapamoja na wawekezaji katika Sekta ya Afya.
Kauli mbiu ni “Ni
jinsi gani tunaweza kufikia malengo ya kuimarisha upatikanaji wa Afya bora kwa
kuunganisha tafiti za kisayansi,ubunifuna Sera za Afya”
Kamati ya maandalizi inaundwa na taasisi saba zikiwemo Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),APHTA,Christian Social Services Commision (CSSC), Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), na Tindwa Medical and Health Services.
Aidha Mkutano wa mwaka huu utahusisha vipengele mbalimbali ikiwemo vikao vitakavyogusia mada kama maendeleo ya huduma za afya,hotuba kutoka kwa wataalamu wazoefu wa afya,kuwasilisha matokeo ya uchunguzi wa majadiliano katika vikundi na maonyesho maonyesho ya huduma na bidhaa kutoka kwa wasambazaji wa huduma za afya na mashirika ya Umma na binafsi.
"ningependa kutoa wito kwa wadau wa afya kutoka serikali na mashirika binafsi,mahospitali,asasi zisizo za kiserikali,taasisi za kitaaluma,watengenezaji wa bidhaa za afya,wasambazaji,wawekezaji na washirika wa maendeleo kushiriki kikamilifu katika mkutano wa mwaka huu" amesema Katibu Mkuu wa taasisi hiyo Rebecca John.
Mkutano huo unatoa fursa chache za udhamini na maonyesho,kushiriki katika mkutano wa mwaka huu kwa kujaza fomu ya maombi inayoweza kupakuliwa kupitia tovuti ya www.ths.or.tz.
by Peter Spirit
Post Comment
No comments