Usikose Hizi Hapa

RAIS MAGUFULI AANDIKA HISTORIA KWA KUWASAMEHE WAFUNGWA 61 WALIOTAKIWA KUNYONGWA

Rais wa Tanzania John Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo amewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.
Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na makosa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara baada ya tangazo lake.
Wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao. Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha.
Miongoni mwa wafungwa waliosamehewa ni Wasanii wenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Nguza Viking (Babu Seya) na mtoto wake Johnson Nguza (Papii Kocha) waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha.

No comments