SERIKALI YA YAPATA MKOPO KWA AJILI YA UJENZI WA BARABARA
Serikali ya Tanzania imepata mkopo wa Shilingi
Bilioni 630.25 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-AFDB na Mfuko wa Maendeleo
ya Afrika-ADF kwa ajili ya mradi wa barabara unaoitwa TSSP yenye urefu wa Kilometa
402.979.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa kiwango cha Lami wa
barabara za Tabora-Koga-Mpanda yenye urefu wa Kilomita 335 na barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye
urefu wa Kilomita 67 ambapo Serikali itachangia Shilingi Bilioni 72.72.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini-TANROADS,PATRICK MHEGALE katika hafla ya
utiaji saini wa mikataba minne,kati ya TANROADS na wakandarasi wanne
walioshinda zabuni ya ujenzi wa mradi huo.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa
MAKAME MBARAWA ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo,amesema mradi huo
ni wa kihistoria kwani tangu TANROADS
ianzishwe hakujawahi kusainiwa mkataba barabara wenye urefu wa kilomita 402.
Hata hivyo
Profesa MBARAWA amewaonya wakandarasi hao kutofanya udanganyifu wowote na
kuwataka waharakishe ujenzi wa miradi hiyo ndani ya miezi 36 .
No comments