Usikose Hizi Hapa

Azam FC yapata mbadala wa Aishi Manula

Golikipa wa Mbao FC, Benedict Haule  akisaini katika klabu ya Azam FC
Klabu ya soka ya Azam FC imekamilisha usajili wa aliyekuwa golikipa wa Mbao, Benedict Haule.
Haule amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo kuanzia msimu huu mbele ya Meneja Mkuu Abdul Mohamed sambamba na Meneja wa timu hiyo, Phillip Alando.
Usajili wa kipa huyo unamfanya aweze kurudi tena kuchezea Azam kwa mara ya pili kwa kuwa ndio timu iliyomlelea katika maisha yuake ya soka kabla ya kwenda kuichezea Mbao msimu uliopita.
Kusajiliwa kwa Haule kunaifanya Azam kufikisha idadi ya wachezaji wanne ambao imewasajili kipindi hiki kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao akiwemo Mbaraka Yusuph na Wazir Junior na Salmin Hoza.
Hata hivyo benchi la ufundi la timu hiyo limeamua kuwapandisha wachezaji wake sita wakiwemo mabeki, Abbas Kapombe, Abdul Omary, Godfrey Elias na Ramadhan Mohammed, kiungo ni Stanslaus Ladislaus, pamoja na mfungaji bora ligi Daraja la Kwanza Yahaya Zaidi.

No comments