Usikose Hizi Hapa

Hii nchi tumerogwa na nani? – Rais Magufuli (+Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo amekabidhiwa ripoti ya pili ya mchanga wa madini (Makinikia), ripoti ambayo imeibua madudu kibao ikiwemo taarifa za kutosajiliwa kwa makampuni mama yanayohusika na uchimbaji wa Madini nchini na kusema Watanzania tumerogwa na nani mpaka turuhusu uozo huo utendeke.


Rais Magufuli amesema kuna wanasheria wengi wasomi lakini wakiingia kwenye kusaini mikataba ya madini wanasahau kabisa majukumu yao na kusaini kwa manufaa yao na sio kwa maslahi ya Watanzania.
Wanasheria wapo wengi wamefundisha na akina Profesa Kabudi sifahamu alikuwa anawafundisha nini? wakiingia kwenye mikataba (Madini) kama hii ile sheria yote inapotea wanasaini chochote wanachoambiwa, na saa nyingine baadhi ya Contract zinatoka zimeandaliwa kule wao wanakuja kuinishwa!! This is the Country! tumerogwa na nani?” Alihoji Rais Magufuli huku akiwaomba viongozi wa Dini watuombee Watanzania.
Basi kama tumerogwa mtuombee nyinyi wachungaji, Mapadre, Mashekhe kama ni mapepo basi yaondoke“amesema Rais Magufuli.
Tazama hapa chini hotuba yote ya Rais Magufuli baada ya kukabidhiwa ripoti ya pili ya mchanga wadhahabu aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya kuchunguza Makinikia awamu ya pili, Prof. Nehemia Osoro.


No comments