Cheko la Maromboso wa Yamoto Band na safari ya WCB (Video)
Muimbaji Maromboso ambaye alikuwa Yamoto Band anadaiwa kuwa yupo mbioni kuelekea kwenye label kubwa ya muziki ya WCB.
Maromboso, Diamond na Aslay
Tetesi hizo zilichukua sura mpya wiki chache zilizopita baada ya muimbaji huyo kuonekana kuwa karibu zaidi na rais wa WCB, Diamond Platnumz hasahasa baada ya kuonekana kushiriki kwenye project ya Diamond Karanga.
Muimbaji huyo akizungumza na Bongo5 wiki hii alikanusha taarifa hizo licha ya suala hilo kuonekana lina ukweli ndani yake.
Hata hivyo watu wakaribu wa muimbaji huyo wanadai muimbaji huyo tayari ameshasaini mkataba na label hiyo na kinachosubiriwa ni wakati wa kutoka tu.
No comments