Tarajia kutazama mechi za klabu bingwa Ulaya (UEFA) kupitia Facebook
Kampuni ya Facebook Inc ipo kwenye mazungumzo na Kampuni ya 21st Century Fox Inc ya kuonesha mechi za Klabu bingwa barani Ulaya kupitia mtandao wake wa Facebook kuanzia msimu mpya ujao unaotarajiwa kuanza mwezi Septemba.
Facebook wamefikia makubaliano hayo kwa kutumia Channel ya Fox Sports ambapo watazamaji wataanza kuona mechi zote za Klabu bingwa barani Ulaya mubashara kupitia mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya bilioni 2 duniani.
Facebook wamefikia makubaliano hayo kwa kutumia Channel ya Fox Sports ambapo watazamaji wataanza kuona mechi zote za Klabu bingwa barani Ulaya mubashara kupitia mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya bilioni 2 duniani.
Kwenye makubaliano hayo Facebook itachukua mkwanja wote wa matangazo yatakayoingia kipindi mechi hizo zikirushwa ingawaje kampuni ya Fox haijaweka wazi ni kiasi gani imelipwa na Facebook.
Mtandao wa Facebook umefikia maamuzi hayo baada ya kuona idadi kubwa ya watumiaji wake kufuatilia michezo ambapo mwaka huu fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya kati ya Juventus na Real Madrid ilitazamwa na watu milioni 3.7 na zaidi ya maoni milioni 98 .
“Mpira wa miguu unakuwa na msisimko zaidi unapokuwa live lakini vipi kama ukiwa peke yako huku ukihitaji maoni ya wenzio au kupongezana na mashabiki wenzio? hii tumeona ni vyema tuwaletee wateja wetu kitu ambacho wataangalia live na kutoa maoni yao hapo hapo hii itapunguza gharama kwa watumiaji pia itakuwa ukomo wa TV“,amesema Sheryl Kara Sandberg Afisa Mkuu mwendeshaji wa Kampuni ya Facebook Inc.
Mwanzilishi na CEO wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg
Kwa upande wa Kampuni ya FOX hao wamesema tayari walianza mapema kuwapa vionjo wateja wao hususani wafuatiliaji wa kurasa zao za Fox Sport kwa kuwapatia kipindi cha weekly soccer show na kuahidi kuwa kwa sasa vitu vyote vitakuwa live na watafunga baadhi ya channel zao zilizokuwa zinaonesha michuano hiyo.
“Kuna mechi nyingi sana zinachezwa Uingereza na ligi ya Hispania kuliko hata idadi ya Channel zetu ambazo tunazitumia kurusha mechi hizo lakini kwa sasa mtumiaji wetu atapakua App moja tu na kutazama mechi azipendazo”,amesema David Nathanson, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Biashara cha Fox Sports.
Miaka mitatu nyuma mtandao wa Facebook uliingia ubia na baadhi ya vituo vikubwa vya Runinga vinavyoonesha michezo kwa kuweka Video zao kwenye mtandao huo kwa mapatano mradi ambao umepelekea Kampuni hiyo kuongeza Feature ya ‘Video Live’ baada ya kufanikiwa kwa asilimia kubwa.
“Kwa hili la kuonesha mechi kupitia Facebook tunaimani Fox watawafikia mamilioni ya watazamaji wake kwani watu wengi kwa sasa wanatumia muda mwingi mitandao kuliko kwenye Runinga“,amesema Dan Reed mkuu wa kitengo cha michezo wa Kampuni ya Facebook.
Kwa kuanza Facebook wataanza kuonesha mechi za Klabu bingwa barani Ulaya kwa nchi za Amerika ya Kaskazini na baadae kusambaa duniani kote.
No comments