KILICHOENDELEA LEO MAHAKAMANI KATIKA KESI YA WIZI WA MADINI YA ALMAS
Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) umeileza mahakama kuwa, sehemu kubwa ya upelelezi umekamilika bado maeneo machache.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon alimeeleza hayo leo mbele ya Hakimu Hakimu Mwandamizi, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya kutajwa.
Wakili Wankyo amedai wanakamilisha upelelezi katika sehemu ndogo iliyobakia na wamewaelekeza polisi kufanya hill na kwamba tarehe ijayo wataieleza mahakama hatua ya upelelezi ilipofikia
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 26, itakapokuja kwa ajili ya kutajwa
Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 1,118,291.43 sawa na Sh 2,486,397,982.54.
Kalugendo ambaye ni Mkazi wa Kinyerezi na Rweyemamu Mkazi wa Mwananyamala wote ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini.
Wanadaiwa kati ya Agosti 25 na ,31, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, washtakiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiliwa na Wizara ya Nishati na Madini walisababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.
No comments