Usikose Hizi Hapa

Video: Serikali yapeleka asilimia 98 bajeti ya Tume ya Haki za Binadamu


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Ashatu Kijaji amesema serikali ina tambua umuhimu wa Tume ya Haki za Binadam na utawala bora pamoja na majukumu yake huku asilimia 98 ya bajeti kwa Tume hiyo imeshapelekwa.


Dkt Kijaji ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodom, wakati akijibu swali bungeni wa Viti Maalum Mwantumu Dau lililouliza
Je? Serikali ina mpango gani wa kutengea bajeti ya kutosha kwa tume ya Haki za Binadamu ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi?
“Viwango vya ukomo wa bajeti kwa mafungu hutegemea vipaumbele vya Taifa na maoteo ya mapato katika kipindi husika, katika mwaka 2017/2018 ukomo wa bajeti ya tume za Haki za Binadamu na utawala bora ni shilingi bilioni 6 milioni 166 laki 978 elfu ikilinganishwa na shilingi bilioni 3 milioni 557 laki 589 na 200 ya mwaka 2016/2017 ikiwa ni asilimia 42.31, ongezeko hili la asilimia 42.31 inadhihirisha kwamba serikali yetu ina tambua umuhimu wa Tume za Haki za Binadam wa utawala bora pamoja na majukumu yake.”
“Serikali inaendelea kuhakikisha mikakati au ukusanyaji wa mapato ya ndani, ili kuhakikisha kuwa mafungu yote ya kibajeti ikiwepo Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora ili kufanya kazi kwa ufanisi. Napenda kulitaarifu bunge lako tukufu tarehe 1 mwezi wa 6 2017 Muheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli alizindua mfumo wa ukusanyaji mapato ya ndani, ikiwa ni moja wapo ya mikakati ya serikali pia kuimarisha ukusanyaji wa mapato. Aidha serikali itaendelea kutoa fedha kukidhi mahitaji ya mafungu mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa na upatikanaji halisi wa mapato,” alifafanua Dkt Ashatu Kijaji.
Mbunge wa Viti Maalum Mwantumu Dau lililouliza aliuliza swali lingine lililohoji:
Kwa kuwa serikali imeliona na kuanza kulifanyia kazi jambo hili, Je? Muheshimiwa waziri uko tayari kuwa bajeti hii iliyopangwa itapelekwa kwa wakati hatimae tume hii ipate kufanya ufanisi wake?
“Serikali yetu iko tayari kupeleka fedha zote zilizopangwa katika mwaka huu 2017/18 kama ambavyo tumefanya kwa mwaka 2016/2017, mpaka sasa tumeshapeleka asilimia 98 ya bajeti yote ya tume ya Haki za Binadam,” alisema Dkt Kijaji.
“Kwahiyo tupo tayari kama serikali, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi kwamba tunafahamu majukumu na tunatambua umuhimu wake.”
Video:

No comments