Usikose Hizi Hapa

DHAMANA KWA WANAWAKE WALIOVISHANA PETE YAPINGWA

Upande wa Jamhuri umewasilisha hati ya kiapo kuzuia dhamana ya washtakiwa wanne wanaokabiliwa na kesi ya kujihusisha na vitendo vinavyoashiria mapenzi ya jinsia moja na makosa ya kimtandano katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.
Hati hiyo imewasilishwa mahakamani leo Jumatano Desemba 13,2017 na Wakili wa Serikali, Emmanuel Luvinga.

Washtakiwa katika shauri hilo namba 548/2017 ni Milembe Suleiman na Janeth Sonza, mwanafunzi wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza, wanadaiwa kuvishana pete ya uchumba licha ya wote wawili kuwa wanawake.

Wengine ni Aneth Mukuki anayeshtakiwa kwa kufanikisha sherehe za wawili hao kuvishana pete na Richard Fabian anayekabiliwa na shtaka la kusambaza picha za tukio hilo mitandaoni.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Wilbert Chuma anayesikiliza shauri hilo, mawakili wa utetezi wameomba muda wa kuipitia na kuijibu hati hiyo kwa hati kinzani kwa sababu hawakuwa wameipata kabla ya kuwasilishwa mahakamani.

Ombi hilo lilikubaliwa na Mahakama ambayo imeahirisha shauri hilo kwa muda.

Mawakili wa utetezi ni Ogastin Kulwa, Mashaka Tuguta na Jebra Kimbole.

No comments