SERIKALI YAPANGA KUWANUFAISHA WAJASIAMALI WADOGO KUTAFUTA SOKO LA NJE
Serikali imedhamiria kuwasaidia wajasiriamali wadogo
wadogo kutafuta soko la nje kwa ajili ya kufikia uchumi wa kati wa
viwanda nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda,Uchumi na biashara
Mhe,Charles Mwijage katika maadhimisho ya miaka 25 ya Tanzania Growth
Trust [TGT] ambayo awali ilijulikana kama Tanzania Gatsby
Trust.
Mwijage amesema tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa miongoni mwa
changamoto zinazowakabili wajasiriamali na wakulima wadogo wadogo ni mitaji
midogo ,teknolojia duni,elimu,masoko n.k huku akifurahishwa kusikia TGT
inaelekeza nguvu zake zote katika kuhakikisha inawasaidia walengwa kutatua
matatizo hayo kwa kupitia programu mbalimbali kama zilivyoainishwa katika
risala.
"nimetaarifiwa kwamba katika miaka 25 TGT imefanya mambo
mengi sana katika sekta za ujasiriamali,kilimo,fedha (mikopo na uhamasishaji
uanzishaji wa benki za wananchi) elimu ya ufundi na elimu ya juu,sayansi na
teknolojia"
Aidha ameongeza kuwa serikali inatambua mchango wa TGT katika
kuanzisha kitengo cha kuendeleza viwanda vya nguo na pia ameipongeza bodi ya
wadhamini na wafanyakazi wa TGT,ambao wanajitolea kwa hali na mali huku bila
msaada wowote kutoka serikali wameweza kufanya kazi nzuri nchini ambayo matunda
yake yanaonekana dhahiri katika Tanzania Bara na Visiwani.
Kwaupande wake mtendaji mkuu wa Tanzania Growth Trust
,Oliver Lwena, ameeleza lengo la taasisi hiyo ni
kuinua wajasiria mali na wakulima wadogo wadogo
waweze kuongeza kipato chao na kuzalisha kwa ufanisi ili kuweza
kufikia uchumi wa kati wa viwanda .
Taasisi hiyo imekua ikitoa mafunzo kwa vyuo vya kati na vyuo vikuu
kufanya kazi za kijasiriamali pia taasisi hiyo imetoa wito kwa
vijana walioko mitaani kuacha kubweteka na kutumia fursa mbali mbali
zinazotolewa ili kufikia uchumi wa kati wa viwanda.
No comments